Anjella Aeleza Ukuaji Wake Katika Sanaa ya Muziki, Ujio wa Kolabo na Yemi Alade

[Picha: Anjella Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii mpya wa mziki wa bongo Ajnella amekaribishwa kwa kishindo na mashabiki tangia ajiunge na lebo ya Konde Music world Wide. Nyota wenzake wa kike wamemkaribisha Anjella kwenye tasnia ya muziki huku wakimuomba kuwa na uvumilivua kwani tasnia hii huwa na changamoto zake haswa kwa akina dada.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mbosso, Anjella Wang'aa Kwenye Nyimbo Tano Bora Wiki Hii

Katika mahojiano na Efm, Anjella alielezea kuwa yeye ni mzaliwa wa Tabora, Tanga kijijini. Alikua katika mazingira ya kidini ambapo anaeleza kuwa alianza kuimba akiwa darasa la nne akiimba kanisani.

Kufikia kidato cha nne, aliamua kuzingatia masomo yake. Alipomaliza ndipo alirudi sasa kufanya mziki. Alijiunga na mashindano flani ya mziki ambapo babake tu ndio alikubali kusapoti wakati huo ila akabadilika alipoona mwanae hapati mafanikio yoyote pale.

Soma Pia: Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Zake Nandy Zinazovuma Bongo

“Kwa sababu wazazi wangu walikua watu wa dini mimi kuimba kanisani kwake ilikua ni ngumu lakini kwa babangu aliniruhusu wakati nmeliza form 4 sasa napambania mashindano, babangu alinisapoti lakini baada ya kuona hakuna mafanikio akawa ananizuia...” alisema kwa kiasi

Tunapoendelea kujua zaidi kuhusu msanii huyu wa kike, mkurugenzi mkuu wa Konde Music Worldwide Harmonize ameweka wazi kuwa kuna wimbo unakuja kati ya Anjella na msanii wa kike kutoka Nigeria Yemi Alade .

 

Leave your comment