Nyimbo Mpya: Nacha Achia Wimbo Mpya ‘Moto’ Akimshirikisha Nay Wamitego

[Picha: Nacha Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa muziki wa Hip-hop kutoka Tanzania Nacha ameachia ngoma yake mpya ‘Moto akimshirikisha Nay wa Mitego .

Huu ni wimbo wa kujisikia vizuri juu ya jinsi maisha yanavyokwenda. Nacha anajivunia kuwa bora kwenye mchezo wa muziki wake huku akitilia maanani maadili yake.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Meja Kunta Aachia Video Mpya ‘Madanga ya Mke Wangu’Akimshirikisha D Voice

“Toto za machizi kamatia, wakinyea kambi kanyagia, Soda na togwa no bia, Ni uoga na Mbegu ili ikue namwagia, Bapa mbona watalia, Samatta Toka tanzania, Nacha nacha kachanjiwa, Kwaiyo basata na Nyinyi mtafungiwa…” hii ni baadhii ya mistari katika wimbo huu.

Pakua Nyimbo zake Nacha Bure Kwenye Mdundo

Video ya wimbo huu imetengenezwa vizuri na kwa urahisi sana kwani ilifanywa ndani ya studio.

Kazi hii ni yake ya kwanza kutoka mwaka huu. Vile vile Nay Wa Mitego anadhihirisha ubabe wake katika wimbo huu anapoimba kwa kuomba wimbo huu utambe na ujisifie bila ya kusukumwa.

Kwa upande wake, anaonyesha kuwa wimbo huu ni moto na hamna atakaye sema mabaya kuhusu hili ngoma.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mbosso Aachia Albamu yake Mpya ‘Definition of Love’

Kwingineko wimbo huu umeandaliwa na Kitonzo huku mchanganyiko wa mdundo huu ukimaliziwa na Chizan Brain. Video hii nayo ikielekezwa na Beel wa Kiri Records iliyoko Dar es Salaam Tanzania.

Kufikia sasa ‘Moto’ umepokelewa vizuri na mashabiki na watazamaji wake katika mtandao wa YouTube wakiendelea kuongezeka.

https://www.youtube.com/watch?v=pJL7qQYPu_c

 

Leave your comment