Anjella Kuachia Wimbo Mpya ‘Kama’ Akimshirikisha Harmonize

[Picha: Anjella Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Anjella kutoka lebo ya Konde Music World wide aliyetambulishwa leo ataachia kazi yake ya kwanza leo usiku.

Kupitia mtandao wa Insatgram bosi wake Anjella; Harmonize, ametangaza ujio wa wimbo wake wa jina ‘Kama’.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Kumi Bora Tanzania Februari 2021

Hii itakua kazi yake ya kwanza kabisa baada ya kutambulishwa kwake rasmi kama msanii mpya wa mziki wa bongo.

Kwenye wimbo huo, anamshirikisha Harmonize.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Collabo 5 Zake Diamond Zinazovuma Bongo [Video]

“Nakukaribisha kuusikia wimbo wangu Wa kwanza ft TEMBO “Kama.” Aliandika Ajella Kwa upande wake Harmonize ametangaza ujio wa wimbo huu huku akimsifia dada Anjella na kumkaribisha rasmi kwenye lebo yake. “The first single under (KMW) wenda huu wimbo ukawa wimbo wako wa kihistoria!!! Maana ndio unaenda kusimika number 1 katika nyimbo nyingi zinazo tarajiwa kusikika na ulimwengu kutoka kichwani kwako!!!! I'm super proud kuwa chanzo cha safari hii ya Anjella naamini katika uwezo wako na leo hii saa 1:00 usiku najua nusu ya Africa Mashariki yote.!!! Kama sio robo 3 wataungana nami kuku simika umalkia kati ya malkia wenzako !!!!All the best.” aliandika Harmonize

Anjella alikua msanii alifanya nyimbo za wasanii baadaa ya wao kuziachia (cover songs). Hivyo Harmonize alipata kumjua Anjella kupitia Instagram wakati Anjella alifanya kuimba wimbo wake ‘Wapo’.

Soma Pia: Pakua Mixtape 5 Mpya za Muziki Bora Machi 2021

Harmonize akaona radhi kukutana na Anjella na sasa ametambulishwa rasmi hii leo kwenye hoteli ya Hyatt.

Mbele ya waandishi wa habari alisaini, mkataba wake na Konde Music worldwide.

Leave your comment