Diamond Platnumz: Nilijifunza Muziki Kupitia Nyimbo Zake Barnaba Classic

[Picha: Barnaba Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nyota wa muziki kutoka Tanzania Diamond Platnumz amemshukuru mwimbaji mwenzake Barnaba Classic kwa kutoa nyimbo zilizo mshawishi kuingia kwenye sanaa ya muziki.

Akizungumza jatika hafla ya kuzindua lebo mpya ‘Next Level Music’ ya msanii Rayvanny, Diamond alisema kuwa alijifunza kuimba kwa kutumia nyimbo za Barnaba.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Zake Nandy Zinazovuma Bongo

Alielezea namna Barnaba alimfunza kucheza guitar mara ya kwanza katika semina waliokuwa pamoja. Baadaye kidogo , iamond akamuona Barnaba kafanya mziki na ametoka sana. Hivyo kwake akachukulia changamoto kufanya uandishi wake huku nyimbo za Barnaba zikiwa motisha ya uandishi wake.

“…Kutafuta tonation ya kuimba nimetafuta kupitia nyimbo zake…kwa sababu wakati nilianza kuimba ilikua sijui niimbe vipi. Hivyo kupitia nyimbo za Barnaba…wakati naanza kufanya wimbo wangu wa kwanza n “Kamwambie” naimba wimbo wote nafikiria tu Barnaba ile …Nenda kamwambie aha jinsi navyo mpenda lakini tatizo bado…namsika Barnaba kasema … Na kama mapenzi bado,,na hivyo nilirudi studio nikabadilisha….” alisema Diamond.

Diamond alizidi kumsifia Barnaba akisisitiza umuhimu wa kukumbuka ulipoanzia kila siku.

Soma Pia: Mixes Tano Bora za Kupakua Kwenye Mdundo Wiki Hii

Vile vile Barnaba alitumia fursa ile kumshukuru Diamond kwa heshima ile huku akielezea umuhimu wa kuendeleza uhusiano mzuri kati ya wasanii wote.

“Hii story ya Nasibu inatifundisha kitu kimoja muhimu kinachoitwa permanent relationship communication…we need to focus…” alisema Barnaba kwa kifupi.  

Leave your comment