Alikiba Apiga Kambi Nigeria kwa Shughuli ya Albamu Yake Mpya

[Picha: Rudeboy Twitter]

Mwandishi: Branice Nafula

Tumia Rafiki Kwenye WhatsApp

Kwa siku kadhaa sasa mkurugenzi mkuu wa Kings Music Alikiba amekua nchini Nigeria kwa shughuli za mziki.

Alikiba amechapisha picha na video kadhaa kwenye mtandao wa Instagram ambapo inasemekana kuwa anashughulikia ujio wa wa albamu yake mpya inayotarajiwa mwaka huu 2021.

Soma Pia: Alikiba’s Top 3 Collabos of 2021 [Videos]

Katika mtandao wake wa Twitter mnamo tarehe 9 mwezi wa pili, Alikiba aliandika kuwa atakuwa Lagos kwa wiki mbili kwa shughuli ya albamu yake. “Lagos for 2 weeks!Album almost done.”

Download Alikiba Music for Free on Mdundo

Kwingineko ni kuwa, mwimbaji huyo wa ‘Infidele’ ashakutana na wasanii maarufu kutoka Nigeria ambao inatarajiwa kuwa watakua na ushirikiano kwenye albamu hiyo.

Wasanii aliokutana nao ni kama vile Praiz na Rudeboy wa Psquare huku Jumatatu hii ameonakana na msanii mwingine almarufu Patoranking.

Alikiba na Patoranking wameonakana kuwa na ukaribu mzuri sana huku wakionekana wakistarehe pamoja na kuimba wimbo wa Alikiba ‘Aje’.

Soma Pia: Nyimbo 5 za Mapenzi Unazofaa Kuskiza Wiki Hii

Kupitia ukurasa wa Instagram kwenye mtandao wa Kings Music, picha ya Alikiba na Patoranking wakiwa pamoja ni dhihirisho kuwa wawili hao wanafanya kazi kwa pamoja.

Hivyo, mashabiki wanatarajia uzinduzi wa album hiyo na pia kujua jina ya kazi hii mpya. Wasanii wengine wanaotarajiwa kuachia album mwaka huu ni pamoja na Mbosso na Diamond Platnumz kutoka WCB.

Leave your comment