Nyimbo 5 za Mapenzi Unazofaa Kuskiza Wiki Hii

[Photo Credit:Alikiba Instagram]

By Branice Nafula

Share on WhatsApp

Mziki wa Tanzania kwa muda mrefu umetambulika kama wa mapenzi kwa wingi. Wanamziki wa Bongo hutunga mashairi haswa kwenye maudhui ya mapenzi. Hivyo nakala hii inaangazia nyimbo tano za mapenzi unazofaa kuskiza wiki hii:

Infidele - Alikiba

Huu ni wimbo wa mwanamuziki Alikiba ambao unaangazia namna mpenzi wake alimhadaa kwenye mapenzi yao. Neno ‘Infedele’ ni la kifaransa ambalo limetokana na neno la kiingereza Infidelity - ambalo kwa kiswahili humaanisha kukosa uaminifu kwa mwenza kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Read Also: Alikiba Drops New ‘Infidele’ Video

https://www.youtube.com/watch?v=7MTwbQB7q5k

Number One - Nandy ft Joeboy

'Number one' ni wimbo mzuri ambao wapenzi wawili wanaelezea hamu na mapenzi yao kwa kila mmoja. Katika toleo jipya, Nandy anaonyesha ubabe wake wakati anatoa sehemu ya kifungu chake kwa Kiingereza. Kufikia sasa huu ni wimbo wenye watazamaji zaidi ya milioni moja nukta moja.

Read Also: Alikiba’s Top 3 Collabos of 2021 [Videos]

https://www.youtube.com/watch?v=8fO1swbTvQk

Nimpende - Ibraah

Hii ni mojawapo ya nyimbo tatu za Ibraah almarufu ‘Karata Tatu’. Nimpende inaangazia namna mapenzi yafaa kuwa .Ibraah aliachaia kazi hizi tatu kama dhihirisho wa ubabe wake kwenye fani ya mziki aina ya RnB. Kwa sasa wimbo huu una watazamaji zaidi ya laki moja.

https://www.youtube.com/watch?v=E3QIeHua4w4

Sukari - Zuchu

Huu ni wimbo wake wa kwanza mwaka huu. Zuchu ameimba jinsi mapenzi yanavyomfurahisha. Kufikia sasa ni wimbo unapata umaarufu kwa kasi kwenye mtandao wa Youtube. Iwapo wewe ni mtu wakufurahia mapenzi basi ‘Sukari’ ndio wimbo wako kwa sasa.

Read Also: 5 Highly Anticipated Bongo Music Albums in 2021

https://www.youtube.com/watch?v=E2mJ-w_sZ2Q

Nashangaa - Aslay

'Nashangaa' ni wimbo wake Aslay unaongazia namna mapenzi yamemzingua. Kufkia sasa wimbo huu una watazamaji zaidi ya laki mbili.

https://www.youtube.com/watch?v=3-0mCkNTZaM

Leave your comment