Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia Video Yake Mpya ‘All Night’

[Picha: BBC]

Mwandishi: Branice Nafula

Tumia Rafiki Kwenye WhatsApp

Mkurungenzi mkuu wa Konde music Worldwide Harmonize ameachia video ya wimbo wake mpya ‘All night’.

Harmonize aliachia wimbo huu siku ya Wapendanao almaarufu Valentine’s day. Katika wimbo huu alimshirikisha mwimbaji chipukizi wa kike Anjella.

Huu ni wimbo wa mapenzi ambapo Harmonize anamsifia mpenzi wake kwa namna anavyompenda.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Album Mpya 'Sound from Afrika'

Wimbo huu ulifanywa kwa lugha ya Kiingereza iliukafikia mashabiki kote ulimwenguni na sio bara la Afrika mashiriki pekee.

Kanda hii iilitengezwa kisiwani Zanzibar ambapo Harmonize anapania kufanya video mia moja huko ilii kuuza uzuri wa nchi yake.

Ukiiangalia video hii, Harmonize aliweza kuonyesha tamaduni za watu wa Zanzibar na uzuri ulioko huko. Tunamuona akiimuimbia binti mmoja mrembo sana akiwa kwenye piki piki.

Anjella naye anaonyesha ubabe wake wa densi kwenye pwani ya Bahari hindi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Album 4 Zinazofanya Vizuri Bongo Mwaka wa 2021

“This is my first …Official single 2021.Nilisema Nataka kuonyesha Dunia kwamba Zanzibar Tanzania ni Zaidi ya Mexico, Zanzibar ni zaidi ya Brazil…Hellow world we made dat in ZanzibarTanzania….” aliandika haya.

Kanda hii imepokelewa vizuri na mashabiki wake na kufikia sasa ni video iliyo na watazamaji zaidi ya laki moja na kumi na saba kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=D8fmQfzrGgo

 

Leave your comment