Nyimbo Mpya: Lava Lava Aachia EP Yake Mpya ‘Promise’

[Picha: Lava Lava Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Tumia Rafii Yako Kwenye WhatsApp

Msanii wa WCB Lavalava hatimaye ameachia EP yake mpya kwa jina ‘Promise’.

‘Promise’ ni EP yenye maudhui ya mapenzi na imeachiliwa wakati huu ili kuambatana na siku ya wapendanao duniani.

Katika EP hii, Lava Lava amewashirikisha Diamond Platnumz na Mbosso.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Album 4 Zinazofanya Vizuri Bongo Mwaka wa 2021

Kwenye nakala hii, tunachambua wimbo nne zilizo kwenye EP ya promise:

Wale Wale

Huu ni wimbo ambao unatoa tafakari juu ya uwongo ambao hufanyika katika mahusiano.

‘Wale Wale’ inaangazia unafiki ambao watu huleta katika upendo wanapoelezea jinsi walivyoumizwa hapo awali, lakini nia yao kuu ni kufaidika na wewe na kuondoka.

https://www.youtube.com/watch?v=aemTYJwFj54

Basi Tu 

Kwenye wimbo huu, Lava Lava amemshirikisha Mbosso. ‘Basi Tu’ ni wimbo unaolezea namna mtu aliteseka katika mapenzi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Album Mpya 'Sound from Afrika'

https://www.youtube.com/watch?v=uJPNEJ8WY8I

Komesha

Huu ni wimbo wa kusifia uzuri wa upendo. Lava Lava anamsifia mpenzi wake huku akimpea ahadi za kuwa pamoja kwa muda mrefu. “Komesha” ni wimbo anao tumia Lava Lava kumuonyesha mpenzi wake kuwa ni yeye tu atampenda mpaka mwisho.

https://www.youtube.com/watch?v=KO93YVV0KOM

Far Away

Kwenye wimbo huu, Lava lava amemshirikisha mkuu wake Diamond Platnumz. Katika ‘Far away’, wasanii hao wawili wanakiri kuwa wanapenda wapenzi wao n hawangependa kuwa mbali nao.

https://www.youtube.com/watch?v=5JP6Ikdu-K4https://www.youtube.com/watch?v=5JP6Ikdu-K4

Leave your comment