Ben Pol Amsifu Barnaba, Amtaja Kuwa Chuma ya Mziki wa Tanzania

[Photo Credit: Ben Pol Instagram]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Msanii tajika kutoka Tanzania Ben Pol hii leo amezua gumzo mtandaoni baada ya kumumiminia msanii mwenzake Barnaba Classic sifa Kochokocho.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Ben Pol ameandika kuwa Barnaba ndiye Chuma cha muziki wa Tanzania.

Ben Pol aliangazia namna Barnaba Classic kwa muda mrefu amekua mwanamziki mwenye ubabe wa kipekee katika fani hii ya muziki kuanzia uandishi wa nyimbo, kuimba na hata kucheza mitambo ya mziki bila shida.

Soma Pia: Ben Pol Biography, Music Career, Awards, Marriage Net worth and Much More

“Siku ya tatu leo nimekuwa nikifikiria jinsi ya kumuandika huyu Mwamba, leo nimesema sitaki kupatia kuandika, nataka niandike hivyo hivyo ninavyojisikia kuhusu yeye. Kwanza amefanya hit songs zisizopungua 300 za kwake mwenyewe, za kuandikia wengine na zile za kuchangia uandishi kwa watu. Anapiga instruments kibao za muziki, ana-produce, kuhusu uandaaji wa nyimbo zake niulize Mimi, anaweza kutumia hata Miezi 6 au zaidi kuandaa wimbo mmoja, ndio maana sauti na muziki wake vinaishi.

Ame-inspire wasanii wengi mno! hata kama wengine hawatasema leo, Mimi mwenyewe nishawahi kuwa namsindikiza (siku hizi wanaitwa Chawa ) enzi hizo akienda studio kwa Allan Mapigo Masaki ilimradi tu awe ananifundisha maujanja yake ya kuimba na kutunga (enzi hizo yeye alikuwa tayari anajulikana, mimi bado underground nikiwa nasoma Dar Sec. Mwaka 2007). Ifike mahali watu wapewe maua yao wanayostahili, mapeema wayanuse wenyewe kabla haijawa too late wakiwa hawapo…” aliandika kwa kifupi.

Soma Pia: Ben Poll Opens up on Encounter with American Rapper T.I and Possible Collabo

Kwingineko ni kuwa Barnaba anatarajiwa kuachia album yake mpya Iitwayo Refresh Mind hivi Karibuni.

Leave your comment