Harmonize Atamba Kwenye Orodha ya Nyimbo 10 Bora Mdundo Tanzania

[Photo Credit:Harmonize Instagram]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Mkurugenzi mkuu wa Konde Wordlwide Harmonize ni mojawapo wa wasanii wakubwa wa bongo ambao wametamba sana mwaka huu wa 2020.

Wiki hii katika nyimbo kumi bora za mdundo Tanzania, wimbo mpya wake Harmonize “Ushamba” upo kwenye nambari ya kwanza.

Download Harmonize Music for Free on Mdundo

Katika orodha ya wiki, Harmonize pia ana wimbo wake wa 'Jeshi' katika nafasi ya tatu na 'Fall in Love' kwenye nafasi ya kumi.

Soma Pia: Harmonize Biography, Music Career, Wasafi Exit, Starting Konde Gang, Top Songs, Relationship and Net worth

Katika mda wa wiki kumi, Harmonize amekua akiongoza orodha hii kupitia wimbo wake wa ‘Jeshi’.

Kwa jumla, lebo ya Konde gang ina nyimbo tano kwenye orodha ya wiki hii. Harmonize alipoachia wimbo wake wa ‘Ushamba’, alitangaza kuwa amememaliza miradi ya kutoa nyimbo mwaka huu.

Soma Pia: Video 5 za Bongo Zinazotamba Mtandaoni YouTube

Wasanii wengine kwenye orodha hii ya nyimbo bora wiki hii kutoka Tanzania ni Diamond Platnumz na Ibraah huku Simi, Patoranking, Master KG na Nomcebo wakiwa wa Kimataifa.

Hii hapa orodha yote yenye nyimbo kumi bora kwenye Mdundo wiki hii:

  • Ushamba - Harmonize
  • Haunisumbui - Diamond Platnumz
  • Jeshi - Harmonize
  • Nitachelewa - Ibraah
  • Jerusalema - Master KG ft Nomcebo
  • Jeje - Diamond Platnumz
  • Jericho - Simi ft Patoranking
  • Baby - JoeBoy
  • Wandoto - Ibraah
  • Fall in Love - Harmonize

Leave your comment