Video 5 za Bongo Zinazotamba Mtandaoni YouTube

[Photo Credit: Harmonize Instagram]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Kila kukicha sanaa ya mziki wa Bongo inaendelea kukua. Wasani wa bongo pia hawajalegeza kamba katika utunzi na uandishi wao shupavu. Katika nakala hii tuanaangazi nyimbo zinazotamba mtandaoni YouTube:

Ushamba - Harmonize

Wimbo huu uliachiwa hivi maajuzi. Kwenye wimbo huu, Harmonize anaangazia watu wengine anaowachukulia kuwa na 'Ushamba' kwa mfano wale wanaofurahi kwenye viungo vya burudani lakini wanawaacha watoto wao na familia wakilala na njaa. Kufikia sasa ni wimbo unaoshika nambari moja kwenye umaarufu na zaidi ya watazamaji millioni moja kwenye mtandao wa YouTube.

Harmonize Biography, Music Career, Wasafi Exit, Starting Konde Gang, Top Songs, Relationship and Net worth

https://www.youtube.com/watch?v=sZ420sDOumE&ab_channel=Harmonize

Rotate - Rommy Jons akimshirikisha Diamond Platnumz

Hii ni mojawapo ya nyimbo kwenye album yake Rommy Jons ‘Changes’. Diamond na msanii kutoka Nigeria Ceeza Mill wameupa wimbo huu umaarufu kufatia ubabe wao katika fani hii ya mziki. Kufikia sasa ni wimbo unatazamwa na wetu wengu huku video ikitarajiwa hivi karibuni. Kwa sasa ni video yenye vikatuni tu iliyotengezwa na visualizer kutoka poka studios na ina watazamaji zaidi ya elfu hamsini na saba.

https://www.youtube.com/watch?v=xkBTeHsMuEY&ab_channel=RjTheDj

Nobody- Zuchu akimshirikisha Joeboy

‘Nobody’ ni wimbo wa kimapenzi ambapo Zuchu anamhakikishia Mnigeria Joeboy kuwa hamna anayempenda kama yeye. Wiki tatu tangu wimbo huu kuachiliwa, wimbo huu unawatazamaji zaidi ya milioni mbili nukta nane.

https://www.youtube.com/watch?v=04Roh3SDyN0&ab_channel=Zuchu

Watani wa Jadi –Rostam wakimshirikisha Mr. Blue

“Watani wa Jadi” ni wimbo unaoangazia timu mbili kubwa zenye mashabiki mahasimu tangia kitambo. Wimbo huu “Watani wa Jadi” unazungumzi namna mashabiki wa timu ya Yanga na Simba FC wanapenda kutaniana na kuangazia namna timu zao ni bora kuliko zingine. Kufikia sasa wimbo huu unawatazamaji zaidi ya laki tano.

5 TBT Bongo Videos That Can’t Age

https://www.youtube.com/watch?v=yQh-Y-DSW9E&feature=emb_title&ab_channel=VIVAROMA

Do Me- Nandy akimshirikisha Bilnass

Huu ni wimbo wa wapenzi wawili wanaelezea namna wanavyo pendana. Wiki tatu baadaye “Do Me” bado unatikisa mitandao na watazamaji zaidi ya milioni moja nukta nne.

https://www.youtube.com/watch?v=enz1B5PuUac&ab_channel=Nandy-TheAfricanPrincess

Leave your comment