TANZANIA: Harmonize Kushirikiana na Yemi Alade, Wizkid Katika Tamasha Kubwa Australia

By Rodgers Omondi

Mwimbaji mashuhuri Tanzania Harmonize pamoja na wasanii wengine waheshimika Afrika, Yemi Alade, na Wizkid wameandaliwa tamasha nchini Australia.

Wasanii hao watatu watawatumbiza mashabiki wao tarehe11/10/2019 and tarehe 12/10/2019 katika tamasha liitwalo ‘Dance Africa’.

Tamasha hilo lililoandaliwa na kampuni ya Taliberry Entertainment litafanyika katika miji ya Sydney na Melbourne.

‘Dance Africa’ ni tamsha la kihostoria kwa kuwa ni mara yake ya kwanza kufanyika mjini Melbourne.

Kwingineko, wasanii watajika nchini Tanzania chini ya kampuni ya kurekodi muziki ‘Wasafi Classic Baby’ maarafu kama WCB watakusanyika Musoma wikendi hii kwa tamasha la Wasafi Festival.

Tamasha hilo litahudhuriwa na Diamond Platnumz, Mbosso, Rayvanny, Lava Lava, Young Killer, Queen Darleen, miongoni mwa wengine.

Wasafi Festival ni moja wapo ya tamsha kubwa zaidi kuandaliwa nchini Tanzania. Tamasha hio huwapa wanamuziki chipuka nafasi ya kutumbuiza mashabiki na kuonyesha vipaji vyao.

Mwaka uliopita, tamasha hilo liliandaliwa nchini Kenya.

Leave your comment