TANZANIA: Vanessa Mdee, Nandy Wateuliwa kwa Tuzo za AFRIMMA

By Rodgers Omondi 

Wanamuziki mashuhuri wa Tanzania Vanessa Mdee na Nandy wameteuliwa kama wagombezi katika tuzo za AFRIMMA.

Wanamuziki hao wametuuliwa katika kitengo cha mwazumiki wa kike bora katika eneo la Afrika Mashariki.

Vanessa na Nandy ni miongoni mwa wanamuziki wengine nane wanaogombea tuzo hilo. 

Download Nyimbo za Vanessa Mdee for FREE 

Wanamuziki wengine walioteuliwa ni kama vile; Vinka (Uganda), Victoria Kimani (Kenya), Akothee (Kenya), Sheebah Karungi (Uganda), Fena Gitu (Kenya), Knowles Butera (Rwanda), Rema Namukula (Uganda), na Juliana Kanyamozi (Uganda).

Nandy alinishinda tuzo hilo mwaka wa 2017, na amewasihi mashabiki wake kumpigia kura.

Kama kawaida watu wangu turudishe kombe nyumbani kwa mara nyingine tena VOTE! VOTE! VOTE! VOTE,” Nandy aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kwengineko, mwanamuziki huyo anaanda tamasha la Nandy Festival ambalo litafanyika kuanzia tarehe 16 Agosti hadi tarehe 17.

Tamasha hilo litafanyika katika Kahama Uwanja wa Taifa, nchini Tanzania.

Download Nyimbo za Nandy for FREE 

 

Leave your comment