Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
TANZANIA: Sababu Za ZaiiD Kubadili Muziki Wake, ‘Nimekuzwa Na Bolingo’
22 June 2018

Rapper ZaiiD amefunguka sababu ya kubadili aina yake ya muziki ambayo alikuwa akiifanya kwa kipindi kirefu.
ZaiiD ambaye leo June 22, 2018 ameachia ngoma mpya ‘Picha’, ameiambia XXL ya Clouds FM kuwa amekuzwa na aina nyingi za muziki, hivyo anaweza kufanya zaidi nje ya rap/hip hop.
“Mimi nimekuzwa na Bolingo, kwa hiyo ukiwa unarap haimaanishi hauwezi kufanya kitu kingine au huwezi kuwa mshabiki wa kitu kingine.” amesema.
ZaiiD ameendelea kwa kusema amekuwa akihamasishwa na miziki mingi, hivyo akachukua mwiitikio huo na kuupeleka katika aina nyingine ya muziki.
“Nimegundua watu wako serious kuna miziki mikubwa sana ya inspirational lakini mwisho wa siku masikini huwezi kila siku kumuhubiria umasikini wake, kuna muda lazima atulie na afurahi pia,” amesema ZaiiD.
Wimbo mpya wa ZaiiD ‘Picha’ unatoka ikiwa ni zaidi ya miezi tisa imepita tangu alipotoa ngoma yake iitwayo Wowowo ambayo imefanya vizuri zaidi ukilinganisha na ngoma zake nyingine za hapo awali.
Source: bongo5.com
Weekly Top 10 songs

In My Bed2:50
KAPEKE LONDON2:23
BIkola2:58
Buwooma2:44
Baddie remix feat Shannnon, aaronix, Tojo3:14
Paver2:55
Nitampeleka kwa Mama (ft. Xouh)3:44
Ex Nkubilako ft DonMusa2:55
CHAMPION GAL3:00
Kamwambie3:47
Top stories
- UPCOMING EP FROM EMKAY64
14 May
- Daniel Sifuna
14 May
- Generation
16 May
- NEW SONG ALERT
16 May


Leave your comment