Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
TANZANIA: Young Dee Afunguka Mpango wa Kumsaini Young Killer
5 June 2018

Msanii wa muziki wa hip hip, Young Dee amefunguka kuzungumzia post ambayo aliiweka mitandaoni inayohusiana na kutaka kumsaini rapa Young Killer Msodoki ambaye kwa sasa anafanya kazi chini ya label ya Wanene Entertainment.
Dee ambaye kwasasa anafanya kazi na label ya King Cash, kupitia instagram aliandika “Hahaha siku ya kwanza ofisini wakati nataka kumsign mdogo wangu #youngkillermsodokii ni kweli anachana sana kijana ana kipaji!,”
Baada ya kauli hiyo Bongo5 ilimtafuta na kuzungumza naye kuhusiana na kauli ambapo alidai hakuna kitu ambacho kinashindikana kwenye hii dunia.
“Young Killer ni rapa mzuri sana, namkubali sana lakini ishu za kumsaini ni mapema sana pale niliandika kama masihara lakini mimi nadhani ni jambo ambalo linawezekana kama nikiamua kwa sasabu ana kila kitu,” alisema Young Dee.
Young Dee na Young Killer wote kwa pamoja watashiriki katika tamasha kubwa la muziki la Sports Muziki Festival linalotarajiwa kufanyika Mwanza, Geita na Kahama katika ya mwezi huu.
Source: bigeye.ug
Weekly Top 10 songs

Trust No One3:13
chile-one-so-lucky4:02
Kamwambie3:47
Joy Is Coming3:08
Buwooma2:44
Udede Ft Msomali x Malume & Samas Alifata Hela Remix6:34
Msaliti 11:25
Leo3:39
Maringo4:00
NANI ft. Kamanda Pedeshee3:56
Top stories
- The Marathon
25 April
- Who Is Bad Beric
24 April
- Cashout by monyzoh boy
24 April


Leave your comment