Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
TANZANIA: Namshukuru Sana Alikiba Kwa Kuimba Wimbo wa Kunitukuza – Yvonne Chakachaka
17 May 2018

Msanii mkongwe wa muziki kutoka Afrika Kusini, Yvonne Chakachaka amesema amemmwagia sifa muimbaji wa ‘Mvumo wa Radi’ Alikiba kwa madai ni msanii mwenye kipaji cha hali ya juu.
Akiongea na Clouds FM, Jumatano hii Chakachaka amesema wimbo huo ambao amefanya AliKiba ni wimbo ambao unawatetea akina mama.
“Mimi na Ali tumeandika wimbo pamoja, una vibe ya “Mkomboti” na tumeimba kwa Kiswahili. Ali yupo comfortable sana kuimba kwenye kiswahili na alinifundisha kiasi kidogo cha Kiswahili.”
Aliongeza, “Wimbo wenyewe unawatukuza wanawake, akina Mama – Ali anaonekana ni kijana mzuri sana na namshukuru sana kwa kuimba wimbo wa kunitukuza mimi kama Mama na wanawake wengine Afrika.”
Chakachaka yupo nchini Tanzania kwaajili ya shughuli za kijamii.
Source: bongo5.com
Weekly Top 10 songs

BIkola2:58
KAPEKE LONDON2:23
In My Bed2:50
Buwooma2:44
Baddie remix feat Shannnon, aaronix, Tojo3:14
Paver2:55
Ex Nkubilako ft DonMusa2:55
CHAMPION GAL3:00
Nitampeleka kwa Mama (ft. Xouh)3:44
Joy Is Coming3:08
Top stories
- Daniel Sifuna
14 May
- UPCOMING EP FROM EMKAY64
14 May
- NEW SONG ALERT
16 May
- Generation
16 May


Leave your comment