Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
KENYA: Nyashinski Aweka Wazi Ujio Wa Kolabo Yake Na Jux
7 May 2018
Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Nyashinski ambaye kwa sasa anafanya vyema na ngoma yake ‘Bebi Bebi’ amefunguka kwa kusema kwamba ana kolabo yake inakuja na muimbaji wa Tanzania, Jux.
Muimbaji huyo ameyasema hayo wiki hii wakati akizungumza na BBC kuhusu ujio wa kolabo zake na wasanii mbalimbali wa Afrika Mashariki.
Nyashinski amesema kwa Tanzania tayari amefanya kolabo na AY ambayo kwa sasa inapatikana katika mtandao wa YouTube.
“Nilifanya kolabo moja na AY ilikuwa inaitwa ‘More in More’ ukiitafuta YouTube utaiona,” alisema Nyashinski. “Lakini nimefanya kolabo na Jux tunangoja tu itoke,”
Alisema kwasasa anatamani kufanya kazi na wasanii wa Uganda na Rwanda kwa kuwa bado hajafanya kazi na msanii wowote kutoka nchini.
Kuhusu kufanya kazi na wasanii wa WCB, msanii huyo amesema bado yupo kwenye mazungumzo na uongozi wa label.
Courtesy: bongo.com
Weekly Top 10 songs

BIkola2:58
KAPEKE LONDON2:23
In My Bed2:50
Buwooma2:44
Baddie remix feat Shannnon, aaronix, Tojo3:14
Paver2:55
Ex Nkubilako ft DonMusa2:55
CHAMPION GAL3:00
Nitampeleka kwa Mama (ft. Xouh)3:44
Joy Is Coming3:08
Top stories
- Daniel Sifuna
14 May
- UPCOMING EP FROM EMKAY64
14 May
- Generation
16 May
- NEW SONG ALERT
16 May


Leave your comment