Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
TANZANIA: Msimfananishe Aslay Na Wasanii Wengine - Chambuso
27 April 2018

Meneja wa msanii wa BongoFleva nchini Tanzania Aslay, Chambuso amefunguka na kudai mwanamuziki wake hataki kushindanishwa na mtu yeyote katika ufanyaji kazi zake na wala haimbi kwa kutegemea kupata sifa kutoka kwa watu wanaomtizama bali anaimba kwa faida yake.
Chambuso ameeleza hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kutokea maneno katika siku za hivi karibuni kwa baadhi ya watu wakidai kuwa kasi ya Aslay kwenye utoaji nyimbo imepungua huku wengine wakidiriki kusema kwamba hata kipaji chake kimeshuka kutokana na kutoa nyimbo ambazo haziwakongi nyoyo kwa upande wao.
"Tunachokifanya sio kibaya ni kizuri kwa sababu sio kila nyimbo ya Aslay utaipenda nyingine utaiona kawaida, tumekupa ngoma mbili chagua moja utakayoona wewe inakufaa. Kwa hiyo mtu akiona kasi ya Aslay imepungua au kutaka na kumfananisha na mtu fulani atakosea, kwa sababu Aslay anafanya muziki wake yeye kama yeye na hataki kushindanishwa na yeyote na wala hafanyi kwa kutaka sifa kwa watu", amesema Chambuso.
Courtesy: eatv.tv
Weekly Top 10 songs

Trust No One3:13
chile-one-so-lucky4:02
Kamwambie3:47
Joy Is Coming3:08
Buwooma2:44
Udede Ft Msomali x Malume & Samas Alifata Hela Remix6:34
Msaliti 11:25
Leo3:39
Maringo4:00
NANI ft. Kamanda Pedeshee3:56
Top stories
- The Marathon
25 April
- Cashout by monyzoh boy
24 April
- MOSS Kay
24 April
- Naphlic_fx
24 April


Leave your comment