TANZANIA: Jide Awafariji Vijana

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye ni mkongwe kwenye game na aneendelea kukimbiza, Judith Wambura au Jaydee, ametoa sababu ya kuandika wimbo wake mpya wa 'Anaweza' ambao amemshirikisha msanii wa Jamaica Luciano.

Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na East Africa Television, Jaydee amesema vijana wengi sasa hivi wamekata tamaa na maisha kutokana na mambo mbali mbali yanayowakabili, hivyo akaona ni vyema iwapo atatunga kitu cha kuweza kuwafariji.

“Vijana wengi sana kwa kipindi hiki wameonakana kukata taa, na kuna vitu vingi ambavyo wanapitia, mambo mengi yamekuwa kelee, party, fake life, nimefikiri ni muda muafaka kuwapa moyo watu ambao wamekata tamaa kuwaambia kuwa wanaweza”, amesema Lady Jaydee.

Kazi hiyo mpya ya Jaydee audio imetengenzwa na mpenzi wake Spice huku video ikitengenzwa na Justine Campos wa Afrika Kusini.

Courtesy: eatv.tv

Leave your comment