TANZANIA: Napenda Sana Hip Hop Hata Kama Naimba – Christian Bella

Muimbaji Christian Bella amefunguka kuhusu mipango yake ya kuanza kufanya muziki wa rap/hip hop.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Lamba Lamba’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio hadi sasa tayari kuna ngoma ameandikiwa na Nikki wa Pili, hivyo muda wowote atasikika akirap.

“Walijua mimi Bella naimba muziki wa Bolingo tu, no!, nani ngoma tayari nimeandikiwa na Nikki wa Pili ambayo nitachana mimi napenda kufanya vitu ambavyo sijafanya ambacho watu hawajajua kama Bela anaweza kufanya hicho kitu,” amesema.

“Napenda sana hip hop hata kama Naimba, napenda sana kusikiliza watu anaochana si Weusi tu nawasikiliza,” ameongeza.

Christiana Bella amekuwa akishirikishwa na wasanii kadhaa ambao wanafanya vizuri katika muziki wa hip hop Bongo, miongoni mwao ni Weusi na Fid Q, pia ameweza kuwashirikisha Joh Makini na Khaligraph Jones kutoka nchini Kenya.

Courtesy: bongo5.com

Leave your comment