TANZANIA: Vanessa Mdee Aungana na Alikiba na Dimpoz Kufuata Nyayo za Ben Pol

Ben Pol ameonekana kuwavutia wasanii wa Bongo Flava kwa mwaka huu katika staili ya kuweka rangi nywele (breach). Baada ya Alikiba na Ommy Dimpoz kufanya hivyo, Vanessa Mdee ameamua kufuata nyayo hizo.

Vanessa amepost picha tatu katika mtandao wake wa Instagram ambazo zinamuonyesha akiwa katika muonekano wake mpya wa nywele zikiwa na rangi ya karoti.

New Hair Who Dis? @iambenpol najua umefarijika sana,” ameandika Vee kwenye moja ya picha alizoziweka kwenye mtandao huo.

Naye Ben Pol amemjibu Vanessa kupitia mtandao huo kwa kuandika, “Happy Faraja Week, naendelea kufarijika tu @vanessamdee.”

Source: Bongo5.com

Leave your comment