Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Msanii huyo amesema kwamba licha ya kuwa maharusi hao wamezawadiwa na kupewa ahadi mbalimbali yeye anafahamu mume wa msanii huyo anapenda sana michezo ya ngumi hivyo atampatia benchi la 'gym', punching bag na vifaa vinginevyo.
"Najua Mwanangu Ashraf (Uchebe) anapenda nini, anapenda michezo ya ngumi. Kwa kulitambua hilo mimi namzawadia mwanangu vifaa vya mazoezi ili aweze kufanya fitness. Ufanye mazoezi ya kupambana hata na kina Mziwanda, sisi watoto wakiume bana tunatakiwa kujilinda pale ambapo inabidi," Billnass.
Shilole na Uchebe walifanya sherehe ya harusi yao juzi Jumapili ambapo ilihudhuriwa na wasanii kibao na wengi wakitoa ahadi ya zawadi mbalimbali ikiwepo elimu na nyinginezo nyingi.
Source: eatv.tv





Leave your comment