TANZANIA: Nandy Afunguka Kufanya Show za Fiesta Bure

Mchumia Juani hulia kivulini. Msanii Nandy amefunguka jinsi alivyoweza kufanya show tano za Fiesta bure mwaka jana kwa kujituma mpaka kumpelekea kuanza kulipwa.

Hitmaker huyo wa One Day, amesema alilia na kuipigania sana hadi kufanikiwa kuipata nafasi ya kutumbuiza kwenye jukwaa la Fiesta mwaka jana, hali iliyompelekea hadi kukubali kuimba bure kwenye tamasha hilo ikiwa ni mara yake ya kwanza kuwepo.

“Kitu kingine ambacho mimi kiliniwia vigumu, I think watu wengi walishangaa kwanini Nandy yupo kwenye fiesta, Nandy ana nyimbo moja ambayo imetoka kipindi cha Ramadhani halafu ikiiisha Fiesta ndio inaanza. Hakuna kitu ambacho nimekipigania kama kile, nilikuwa ninalia asubuhi, mchana na jioni kwa sababu nilikuwa ninaamini kwenye ndoto yangu kwamba nikipewa nikazunguka mikoa yote basi hiyo nitakuwa nimeweza kufanikiwa,” amesema hayo wakati wa kongamano la Her Initiative Jumamosi hii katika chuo kikuu cha Udsm.

“Nilimfuata mimi ofisini bosi nikamwambia mimi ni msanii wako, naomba nijilipie kila kitu hadi ndege ilimradi tu niwepo kwenye tangazo kuwa Nandy naye yupo ataperform. Nikamwambia hivyo yeye akaniambia huwezi Mwanza nauli ni nyingi, mimi nikamwambia ninajua nitatoa wapi hela ni vile tu ili niweze kwenda. Nilifanikiwa nikajilipia kila kitu, madansa wangu, nguo natengeneza mwenyewe nabrand kampuni yangu halafu ninajibrand mimi mwenyewe kwa sababu ninaamini ile oppoturnity ambayo nimeipata itanisaidia baadae,” ameongeza.

Nandy amesisitiza, “Nilipewa Fiesta tatu na kila nikienda “I kill it”, mpaka wakaniita wewe Nandy unajitahidi, tunakupa Fiesta nyingine mbili zinazofuata tunakulipa. Nimefanya hizo Fiesta kwa nguvu zangu zote, nikaanza kulipwa nilivyomaliza Fiesta watu wengi wakaanza kumjua Nandy, kupitia Fiesta na ile opportunity ambayo mimi nilipewa.”

Source: bongo5.com

Leave your comment