TANZANIA: Joh Makini Atoa Somo Hili Kwa Wasanii Wenzake!

Rapa kutoka Weusi anayetamba kwa sasa na 'hit' song ya 'Waya', Joh Makini amefunguka na kuwataka wasanii kujitengeneza 'brand' ili kuweza kupata heshima ya kusaini mikataba minono ya makampuni mbalimbali ili kujiongezea kipato kizuri kupitia sanaa.

Joh amefunguka hayo ikiwa ni kipindi cha muda mfupi tangu kupata shavu la kampuni ya mtandao wa simu akiwa pamoja na wasanii wengine kutoka kundi la weusi  na kudai kuwa siri kubwa ambayo makampuni hutazama kabla ya kutoa shavu ni brand ya mtu wanayetaka kufanya nae kazi

"Msanii lazima utengeneze brand na kuitengeneza siyo mchezo lazima utumie gharama kubwa. Hivyo makampuni yaliyopo nchini ni busara yakatutumia sisi wasanii kutangaza nao kwa sababu ndiyo kazi yetu ya kuburudisha na kufundisha kama jinsi mataifa mengine yanavyofanya kwa wasanii wao. Lakini sasa inabidi wasanii na sisi tuji-brand kuanzia maisha tunayoishi, kuepuka skendo, kuchagua maeneo ya kwenda, marafiki wanaotuzunguka na kuhakikisha unajitengeneza ili kuweza kupata deal kama hizo"- alisema Joh Makini.

Hata hivyo Joh ameongeza kuwa wasanii wengi wana majina makubwa lakini bado hawaishi maisha sawa na brand zao.

Source:eatv.tv

Leave your comment