TANZANIA: Nataka Kuwa Beyonce wa Bongo – Nandy

Msanii wa muziki kutoka THT, Nandy amefunguka kwa kudai kuwa atahakikisha anafanya vizuri katika muziki anaofanya ili afike mbali zaidi kama wasanii wakubwa duniani.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘One Day’, amedai msanii akimuomba Mungu, juhudi katika muziki wake pamoja na nidhamu ya kazi anaweza kufika mbali zaidi.

“Nimemweka mbele Mwenyezi Mungu, pia Watanzania waniweke kwenye sala zao. Nimepanga vitu vingi kwenye muziki wangu nataka kuwa zaidi ya mastaa wa kike Bongo, siwezi kuwaangusha naona ndiyo kwanza naanza, nataka kuwa kuwa Beyonce wa Bongo,” alisema Nandy.

Kwa sasa muimbaji huyo ni mmoja kati ya wasanii wa kike ambao wanafanya vizuri kwenye tasnia ya muziki nchini.

Source: bongo5.com

Leave your comment