TANZANIA: Christian Bella Kuja na Wimbo ‘Shuga Shuga’, Asema ni Wimbo Mkubwa

 

Muimbaji wa muziki wa dance na Bongo Flava, Christian Bella, amesema wimbo wake ujao unaitwa Shuga Shuga.

Ameiambia Bongo5 kuwa wimbo huo ni mkubwa na wenye tofauti kubwa.

“My bro nakuambia ni bonge la ngoma, trust me,” aliambia Bella.

“Ni kidogo ya kucheza, melody, ujumbe, miteremko zile panda na kushuka hatari sana,” ameongeza. “Shuga Shuga Mungu akipenda video ntafanyia nje pia, labda hata nje ya Afrika. Mungu akipenda, mwezi wa nne au wa tano ntakuja na Shuga Shuga.”

Kwa sasa muimbaji huyo anayejiita King of the best melodies, anafanya vizuri na wimbo wake Ollah aliomshirikisha rapper wa Kenya, Khaligraph.

Source: bongo5.com

Leave your comment