TANZANIA: Sipigi Tena Show Chini Ya Millioni 10 - Jux

Exclusive kwenye XXL ya Clouds FM Juma Jux amedrop habari mpya mjini kuhusiana na muziki wake.

Ikiwa ni baada ya Jux kuumiza kinoma noma weekend iliyopita kwenye show ya Love, Melodies & Lights kwa kupiga bonge moja la show pande za Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Jux amefunguka kuwa kuanzia sasa hawezi tena kupiga show kwa gharama ya chini ya millioni kumi za kitanzania.

Jux amefunguka hayo wakati akiambatana na G Nako katika kurelease ngoma mpya ya G Nako ambayo amemshirikisha Jux inayokwenda kwa jina la Go Low.

Source: perfect255.com

 

Leave your comment