TANZANIA: BONGO FLEVA NDIO IMENISAIDIA KUFIKA HAPA - Christian Bella

Mkali wa masauti Christian Bella amedai kuwa muziki wa Bongo Fleva ndio umemsaidia kufika alipo sasa kimuziki.

Muimbaji huyo amesema muziki huo umemsaidia kujifunza vingi na kugundua mapungufu yaliyopo kwenye muziki wa bendi na kutengeneza muziki ambao unaweza kuimba pamoja na mashabiki kwenye matamasha.

“Bongo Fleva ndio imenisaidia zaidi imenifanya mimi kujua natakiwa nifanye nini. Unajua kuna mapungufu tunayo sisi kwenye bendi tunajiimbiaga bila shangwe. Hatuna shangwe kwenye show, nyimbo nzuri watu wanakuangalia na wanacheza, wanakutunza wanakaa lakini kwenye Bongo Fleva nimegundua lazima utengeneze hit inatakiwa mashabiki waimbe, ndio vitu nimejifunza,” amekiambia kipindi cha Dj Sho cha Radio One.

Bella ameongeza kuwa alivyosimama yeye mwenyewe ndio imemlipa zaidi kuliko bendi.

 

Source: bongo5.com

Leave your comment