• Stream Mbosso - Sele Feat. Chley (Uchambuzi)

    Sele Feat. Chley (Uchambuzi)

    Mbosso

    1:33

Msanii mashuuri kutokea Tanzania, Mbosso ameachia video mpya ya kibao chake Sele, huku akimshirikisha mwanadada Chley, msanii kutoka Afrika Kusini.

Kibao hiki ni cha kusisimua mno Kwani kutoka mwanzo kinamnata msikilizaji kwa mdundo unaovutia mtu kiasi cha kuamka na kudensi. Kupitia uandishi wa wimbo huu, Mbosso anajaribu kuelezea tabia ya Sele au Selemani kwa ukamilifu, ambaye ni mtu wa vituko vingi haswa anapolewa. Sele ni kibao ambacho kimechanganya ladha ya muziki ya Bongo Flava kutoka Tanzania na ladha ya Amapiano kutoka Afrika Kusini ambayo imekuwa ikiichukua dunia kwa kishindo.

Kumshirikisha msanii Chley katika kibao hiki, kunatajirisha ubora wake Kwani msanii huyo anawakilisha kwa njia yake ya kipekee ya kufoka katika lugha ya Zulu. Mchanganyiko huu wa ladha hizi mbili pamoja na matumizi ya lugha ya Kizulu kuna changia katika umaarufu wa kibao hiki Kwani kitaenea kupita mipaka ya Afrika Mashariki na Afrika Kusini. Kanda ya video nayo ni ya kuburudisha vile vile huku ikionyesha miondoko ya kupendeza inayoigwa kwenye mtandao wa kijamii wa TikTok. Kupata habari za muziki unaona ha katika bara la Afrika tembelea tovuti ya www.mdundo.com.