Lyrics
eyo kutoka Panorama nasukuma ringi kisomi,
maana wa kufanya hivi simuoni,
na maji ni ya shingo nawapalia madingi kooni,
kwa mistari mingi kushinda hata nzi sokoni
View moreDizasta ndo' jina logo ya mtaa ina-shine kuta,
na-type lugha usongo kushinda mdai fuba,
nuksi kama asili iliyo-design kufa,
shwain kaa kando uone game nai-define upya, yoh!
na usawa ndo' huu sikosei,
mnapotea kwa sababu hamna basics, na hapo ndo'mnayumba,
ndio maana mkienda juu siongei na vikundi vyenu utafikiri
crew za ma-gay, Ski'za
mfumo wa nguzo za hizi tungo ni ishara kwamba nimefuzu,
kwa maana hii miruko ni imara,
niko sky natafuta kikomo, kwenye kisomo
nachora beyond normal muulize Dubo Dibala
expansion to the hyperspace,
nakaanga mawe yanaiva ma-verse,
unaweza 'dhania ni Complex Ngwair ama utadhania Langa rebirth,
material deep huku diver haendi
ni kama mufti aliyelamba haramu,
tumeganda hata kope haiyumbi utasema ameganda sanamu,
sipo kwenye route ya wavuvi mamluki nipo na mafundi
kina Ngugi wanawapa salamu
ukifika uliza utaambiwa mimi ni nani,
utaonyeshwa mtiti kilo nyingi haipimi mizani,
ukishindwa ita wabishi waje wahiji imani
waeleze naurudisha mziki nyumbani
na kama ndo' unafika sasa karibu center ya tenzi, huh!
uone bidhaa bila ya expire date,
kubwa kushinda hata empire state,
so my single line is like your entire verse, nigga
usinishike mkono nikipake,
hatuhitaji shobo, ni vina na mishono ka zuria,
tofauti na midosho ya kipambe,
tofauti na ngono au drama za domo na wenzake
nishavunja mwamba Kaskazini,
Tanzania hakuna Mroma mwenye stamina ya ku-rap na mimi,
mizuka hewani utadhani anaye-rap ni jini,
nusu mtu nusu rap machine
najua ushasikia tenzi bro ebwana utenzi huu noma,
ita wanafunzi waje waperuzi ngoma,
we don't play good ukija tuna-execute
ujuzi kama Sherryl Woods naandika zaidi ya Daily News soma
panda safina imefunguliwa mito,
na kingo ni mbovu ukioga tu umefunguliwa mito,
wenzio wameacha mtindo wa kunichukulia simple,
sikudanganyi hamna hewa huku nilipo
kwa maana ni juu sana hata ukibebwa kusogea bado,
kwa hisia za ushairi napotea angani
kama vile jangwani zinavyopotea nyayo,
Ah! pesa inaongea nami naongea nayo
single nzito utafikiri na-double,
nafoka kwa roho mbaya kama dingi wa kambo,
muulize Fifi niko real kiasi sili na sharo,
ripoti kutoka kilele cha ubora Kilimanjaro
ngoja tu-diverge, thanks to rap I won't die virgin,
mwandiko utasema kau-design shorty,
sura ya kazi utahisi mdai kodi,
rai ya uhai mashakani siku hizi Emcees hawakai road
maliasili mama'angu anailinda kama mtoto wa majini,
unaziamini ndoto? mi'ni kwa mama'ako
ndoto kwa demu wako, hata baba'ako anatamani
kuwa na mtoto kama mimi
sahau kuhusu chips kwenye foil,
hiki chakula cha ubongo cha ku-feed kids
kwa lugha ya ku-twist kama coil,
na maisha yangu myth mpaka naenda deep unaweza hisi nai-discover oil
code zinafanya wazungu wanazunguka,
mafungu wanafunguka, mazuzu wanazuzuka,
nilikuwa mtupu nikaokota buku nikabukuka,
leo nasimulia tungo tukufu ni ka' Lufufu kafufuka
Legend kama Koffi Olomide,
naikamata Dar kama Daudi wa Kolomije,
nawalaza doro si-follow bata na-follow mishe,
na ufundi ni controverse utasema Apollo mission
misele hapa mjini,
natembea na begi la maiti nachinja bila kwere wala nini,
busara tele utasema Nyerere ama Mwinyi,
nafika kilele ila sipigi kelele kama nyinyi
Fuvu limeshiba mautundu kwenye kichwa,
niko underground na huku ndio mitutu inakofichwa,
walikuja na gubu walizikwa kama wafu mbongo tubu,
wazungu wanasujudu hiki kichwa
we ni player unasifika? mi' ni game,
kitambo kama Zinja kwenye plane za Afrika nasikitika hamjui,
messages n'nazo-pack kwenye pictures n'nazo paint,
niki-reveal scriptures kama saint uh!
ni kama big hulk kwenye mini-bus,
sitoshi kwenye skinny vazi
gani lita-fit, ma-emcee wana-sound kama injini yenye hitilafu,
mi'ni king wa Swahili rap get't? (yeeah!!)
wanasema i am too real for the industry,
Stockhom mpaka Italy,
ka' cruise yatch, groove hii ni concord
focus kama msongo ama mnoko anaye-solve murder mystery
(ama' G.O.A.T you can see that) look at my family tree,
look at the chemistry i have, look at my pedigree,
you talk about being competitive? being authentic or
having body of work or longevity?
cheki hizi rythm cheki silabi,
wananiita trickster cheki ma-trickery,
ma-emotions passion love hope sympathy,
uh! utahisi mkono wa Mungu umeandika hii
na-spit holly ka' n'nam-bite Masihi,
kwa heshima namnyang'anganya mic Madee,
hii ni fact hakuna emcee wa ku-rhyme ka' D,
shorwebwenzi nenda uka-bite na hii
ni deep sana na ndio maana wanaita ngumu ku-rap,
deep kama chumvi kwenye uvungu wa ny@p,
kabla hujani-book nitoe kwenye hayo mafungu pumbavu,
mi' sio malaika mi' ni Mungu wa rap
Haleluyah!
Leave your comment