EXCLUSIVE (TANZANIA)- Amini azungumzia suala la ukimya wake kwenye muziki

 

 

 

Msanii Amini amevunja ukimya kwa kuwaondoa wasiwasi mashabiki zake, na kusema kuwa hadi sasa ana nyimbo tano kwa ajili ya mashabiki zake.

Mwanzamuziki huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa alikuwa kimya ili ahakikishe ana nyimbo  zake tano mkononi.

“Nilitaka niwe na nyimbo zangu tano mkononi ndio nianze kuachia nyimbo”, alisema. “Kwasababu nataka niandae vitu vizuri ambavyo vikitoka kwasababu naweza kuchelewa na nikatoa nyimbo na ikafanya vizuri tu. Sina haraka kwasababu ninachokifanya mimi nakiamini kwasababu nimewaandikia wasanii wengi nyimbo na zikafanya vizuri” aliongeza Amini.

Leave your comment