TANZANIA: Ruby amuanika kijana anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake

 

 

Mkali wa wimbo ‘Na Yule’ Ruby ameshare video mbele ya mashabiki wake katika mtandao wa instagram akibusiana na kijana anadaiwa kuwa ni mpenzi wake.

Muimbaji huyo alikuwa msiri kwenye mahusiano yake. Wiki hii amepost picha taofauti tofauti za kijana huyo huku akiandika ujumbe wa kimahaba hali ambayo imewafanya mashabiki wake kuhisi huwenda ni mpenzi wake.

Katika moja ya picha muimbaji huyo aliandika: “Comedian wangu @_mantogoro love you baba nyakunyaku stay away. Katika picha nyingine aliandika “My world” huku akimtag kijana huyo.”

 

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake ‘Wale Wale’ aliouachia wiki chache zilizopita.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment