TANZANIA: Diamond aeleza sababu ya kutokuhudhuria ‘Fiesta’
6 October 2016

Staa wa muziki chini Tanzania Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ aelezea sababu ya yeye kutokuonekana katika tamasha linaloendelea kufanyika nchini Tamasha la Fiesta. Tamasha hilo ambalo linahusisha wasanii mbalimbali nchini Tanzania wanaofanya vizuri na kutamba na nyimbo zinazohit kwa wakati huo..
Kupitia kipindi cha Jahazi kinachorushwa kila Jumatatu mpaka Ijumaa kupitia kitua cha Clouds Fm, Diamond alieleza na kusema kwamba mkataba wake na kampuni ya simu ya Vodacom ndio sababu ya yeye kutoshirikI Fiesta mwaka huu. Tamasha hilo kwa mwaka huu 2016 limedhaminiwa na kampuni ya simu ya Tigo, ambayo ingeleta mgongano wa kimaslahi..
Unaweza kutazama hapa moja kati ya Tamasha la Fiesta lililofanyika mkoani Tanga mwaka huu:
Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz




Leave your comment