TANZANIA: Diamond Platnumz awaambia mashabiki wake wasiamini kila kinachoandikwa magazetini kuhusu yeye
9 August 2016

Licha ya jamii kutegemea sana kupata taarifa mbalimbali kutoka vyombo vya habari vya magazeti, msanii Diamond Platnumz ameonekana kutokuwa na imani na vyombo hivyo hususani magazeti ya udaku kiasi cha kuwaasa mashabiki wake.
Akiongea kwenye mahojiano na runinga ya EATV kwenye kipindi cha eNewz Diamond Platnumz amewaambia mashabiki wake wasiamini kila kinachoandikwa na magazeti kinachomhusu yeye na maisha yake ya kila siku kwani mambo hayo hayana ukweli, na wala kwa sasa hafanyi mahojiano na gazeti lolote.
Diamond ameendelea kusisitza wananchi wafuatilie mitandao ya kijamii kama vile Instagram, facebook, twitter, na snapchat kwani kila kinachokuwa pale kina muhusu asilimia mia moja.
Pamoja na mambo mengine Diamond ameeleza kuwa mara ya mwisho kafanya mahojiano na waandishi wa magazeti ni siku alipokuwa akizindua label yake ya WCB.
Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz




Leave your comment