THE PRODUCER'Z WAJA NA "WIFE MATERIAL"

The Producers,ni kundi la Muziki,linaloundwa na wanamuziki wawili,ambao ni MBATIZAJI pamoja na MAN WATER.Kundi hili limeanza kusambaza wimbo wake mpya unaojulikna kwa jina la "WIFE MATERIAL" katika vituo mbalimbali vya radio vilivyopo nchini Tanzania na nje ya nchi.

Wimbo wa WIFE MATERIAL umerekodiwa katika Studio mbili,FLEXIBLE MUSIC ambayo Producer wa studio hiyo ni MBATIZAJI,pamoja na COMBINATION SOUND ambapo producer wa studio hiyo ni MAN WATER.

Watayarishaji hawa wa muziki,waliamua kuanza kufanya kazi pamoja kipindi cha miaka ya 2004,walipokutana mkoani Morogoro.Na ilipofikia mwaka 2011 waliweza kufanya nyimbo iliyojulikana kwa jina la "HESHIMA KAZI",nyimbo iliyofanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio pamoja na TV.

Baada ya kimya kirefu sasa THE PRODUCERz,wamerudi tena na nyimbo nyengine,ambapo kwa sasa wanasambaza Audio ya nyimbo hiyo,huku wakiwa katika maandalizi ya kufanya video ya wimbo huo hivi karibuni.
WIFE MATERIAL ni nyimbo yenye ujumbe mzuri ambao unaweza kusikilizwa na rika lolote,na ni wimbo unaoburudisha na kufundisha pia.Kwa sasa wimbo huo unapatikana katika mitandao mbalilmbali ya kijamii,na unasikika katika vituo mbalimbali vya radio.

Leave your comment