TANZANIA: Q Chief aitupia lawama uongozi wake

Msanii wa Bongo Fleva Q Chief atupia lawama kwa uongozi wake kwa kushindwa kumsafirisha kwenda kufanya video nje ya nchi kama alivyoahidi mara ya mwisho alivyozungumza na Enewz.


Awali Star huyo wa bongo flava alishawahi kuiambia Enewz kwamba hana mpango wa kufanya kazi na wakina Hanscana yaani madirector wa bongo na plan zake ni kupanda ndege na kwenda kufanya video nje na madirector wengine kutokana na madirector wa Bongo kukosa ubunifu na kuwachana kuwa warudi shule wakasome kwanza.


Sasa lawama za Q Chief zimerudi kwa uongozi wake wa QS Entertainment kuwa kutokana na wingi wa wasanii ndiyo sababu ya yeye kukosa nafasi ya kutimiza mipango yake kama alivyotarajia.

Leave your comment