TANZANIA:Nimeshatumia zaidi ya bilioni 1 kwenye muziki – QS Mhonda
18 April 2016

Mkurugenzi wa lebo ya QS Mhonda Entertainment amesema toka ameanza kusimamia harakati za kimuziki tayari ameshatumia zaidi bilioni 1.
Mfanya biashara huyo wa majengo ambaye lebo yake ya QS Mhonda Entertainment anamsimamia MB Dog , Q Chilla, na Mzee Yusuph pamoja na bendi ya QS International Band ameiambia Bongo 5 jumatano kuwa hela hizo amekuwa akizitumia katika nyakati tofauti tofauti.
“Kusema kweli bado sijarudisha hela yangu na tayari nimeshatumia zaidi ya bilioni 1 kwenye muziki, yaani ni kama nawasaidia tu”, alisema QS Mhonda.
“Kwa hiyo hii ni sehemu ya maisha yangu kwa sababu wakati natafuta hela nilimuomba mungu anipe pesa ili na mimi niweze kuwasaidia watu kama hawa, ndicho nachokifanya sasa hivi”.
Aliongeza, “Mimi nimemsimamia Nay wa Mitego, nikamnunulia gari mpya, H. Baba amepita kwangu. Pia niliwai kumleta hapa nchini JB Mpiana, project ambayo iligharimu zaidi milioni 300. Pia kuna hawa wengine kama akina Mzee Yussuf ambao huwa nawasaidia mara moja moja, kwa hiyo kusema kweli ni gharama kubwa sana”.

QS Mhonda akiwa na Q Chillah




Leave your comment