TANZANIA: Nyimbo yangu ya “Nitasubiri” inaukweli ndani yake - Jux
5 April 2016

Msanii wa muziki wa bongo fleva wa nchini Tanzania, Juma Mussa Mkambala a.k.a Jux amesikika akisema kwamba nyimbo yake ya ‘Nitasubiri’ ilikuwa na ukweli ndani yake. Jux alisema muziki wenye ukweli unaweza ukauimba vizuri zaidi kuliko muziki ambao hauna ukweli.
Msanii huyo aliyasema hayo katika mahojiano yake na Sporah katika kipindi cha The Sporah Show kinachorushwa na kituo cha Clouds hivi karibuni. Jux alisema, “ Yah, ni ya ukweli kwasababu sikua katka hali nzuri. Kitu ambacho kilikuwa kinaongelewa ni kwamba girlfriend wangu alipatwa na matatizo kwahiyo mimi sikua sawa kwa huo muda”. Jux akaulizwa mbona hakusubiri ( akiwa na maana kumsubiri mpenzi wake wa zamani Jacky Cliff), na ndipo msanii huyo akajibu na kusema, “time, mambo yanabadilika. Am young, I have to live the life”.
Kama ulipitwa na video ya 'Nitasubiri', hi hapa:




Leave your comment