TANZANIA: Wake zangu wananivuraga – Mzee Yusuph.

Mkurugenzi wa kikundi cha Jahazi Modern Taarabu, Mzee Yusuph amesema hakuna kitu kinachomuumiza kama kutoelewana kwa wake zake wawili.

Akizungumza katika kipindi cha The Sporah Show cha Clouds Tv, Mzee Yusuph amesema anapitia wakati mgumu sana kuwamiliki wake wawili anaowapenda lakini wao hawapendani. “Kusema ukweli napata wakati mgumu kuwahandle, yani linanivuruga sana hili swala. Ndio maana natamani hata kesho waelewane. Sometimes ni raha hata kama wakiwa hawaelewani maana hata kama nimeenda pahali labda nimezunguka hakuna anayelinda” alifafanua zaidi Mzee Yusuph.

“Lakini hii ni chungu sana, hili kwangu ni tatizo, natamani le kesho waelewane. Tatizo la hawa wote ni watu wa karibu, ndio maana mimi nimeshawaambia kwa midomo yangu, hili jambo nataka liishe , sitaki kusema nataka liishe kwasababu nilishawaomba sana, na ninachoona na ustaa ndio unawowasumbua wanashindwa kujua mimi ni staa zaidi yao”aliongeza Mzee Yusuph.

Mwanzo wa mwaka huu Mzee Yusuph amedai kuwa amewakataza wake zake Leila Rashid pamoja na Chiku wasitumie mtandao wa Instagram kwa madai mtandao huo unakuza ugomvi.

Chanzo: Bongo5

Leave your comment