TANZANIA: “Kuna maisha baada ya muziki”. – Cyrill Kamikaze

 

Hitmaker wa 'Shori' Cyril Kamikaze amefunguka kuhusu suala la muziki na maisha huku akiwataka wasanii wenzake kuto bweteka wakidhani wataishi maisha yao wakiimba milele hivyo wanatakiwa kujiongeza na kujiingiza kwenye masuala ya kibiashara kama afanyavyo yeye. Akizungumza na Planet Bongo ya East Africa Radio hivi karibuni Kamikaze ameeleza kuwa kuna maisha baada ya muziki hivyo kujiandaa mapema ni vizuri zaidi, huku akiongeza kuwa muziki unaweza kubadilika wakati wowote na ukabadili maisha ya msanii.

 

Vilevile Cyril amefungukia ukimya wa kundi la Wakacha linaloundwa na yeye na Jux ,na kueleza kuwa wapo mbioni kuanza project ya pamoja hivyo mashabiki wakae mkao wa kula kwa kuwa kuna nyimbo nyingi na nzuri kwa ajili yao.

 

Kama ulipitwa na video ya 'Shori' ya Cyrill hii hapa:

 

Chanzo: Mtembezi.com

Leave your comment