TANZANIA: Christian Bella apata mtoto wa kiume
16 March 2016

Msanii wa miondoko ya dance Christian Bella amepata mtoto wa kiume wiki iliyopita. Taarifa za msanii huyo kuwa amepata mtoto mwingine ni pale baada ya msanii huyo kupost katika ukurasa wake wa Instagram na kuandika kuwa “ Ahsante Mungu kwa kunipa mtoto nina furaha saaaana. Alizaliwa jana usiku katika hospitali ya Karolisnka, Stockholm, Sweden. Karibu sana my boy Christopher penda wewe sanaaa”.

Mke wa Christian Bella anaishi nchini Sweden. Christian Bella anawatoto watatu ambao ni Jordan (7), Hance (2) pamoja na Christopher ambaye amezaliwa hivi karibuni.
Watoto wa Christian Bella.




Leave your comment