TANZANIA: “Sikujua kama Jackie alikuwa akiuza Unga” -Jux

 

 

Inaonekana kuwa Jux hawezi kuyakwepa maswalli kuhusu Jackie Cliff. Uhusiano wao ulipatwa na doa baada ya Jackie Cliff kukamatwa na madawa ya kulevya Hong Kong ambako hadi leo anatumikia kifungo. Lakini kwa mujibu wa muimbaji huyo, kuwa mpenzi wake alikuwa akijihusisha na madawa hadi kukamatwa ilikuwa ngeni kwake kama kwa watu wengine wote.

 

Jacki Cliff

 

“Kiukweli nilimpenda sana Jackie Cliff maana mara nyingi mimi ninapokua na mtu napenda kweli sababu huwa nahitaji kutulia”, alisema Jux kwenye kipindi cha Mkasi kinachorushwa katika kituo cha East Afrika Tv “Channel 5”.

“Lakini huwezi amini sikujua kama Jackie Cliff anafanya mabo hayo mpka alipopata ndiyo nilijua mimi. Hivyo ilinipa wakati mgumu sana nikawa sijielewi.

Hadi sasa haijulikani ni lini Jackie atamaliza kifungo chake. Jux kwa sasa yuko kwenye mahusiano ya kimapenzi na msanii mwenzake Vanessa Mdee.

 

Jux akiwa na Vanessa Mdee

 

 

 

Chanzo: Bongo5.com

Leave your comment