TANZANIA: “Mapenzi yamenifanya nihamie Australia” – Rama Dee

 

 

Msanii wa muziki wa R&B Tanzania Rama Dee amesema kuwa kilichomfanya ahamie Australia kwa mke wake ni mapenzi na sio kitu kingine.

Akizungumzza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Afrika Radio ijumaa hii, Rama Dee alisema kuwa anampenda mke wake ndio maana akahamia Australia. “Unajua ni mapenzi ndiyo yaliyonifanya nijhamie nchini Australia na hakuna kingine" alisema Rama Dee

Rama Dee katika harusi yake na mke wake

 

"Yaani kiufupi mimi nimeolewa kule maana kwenye mila zetu sisi watanzania huku wanamke ndio anamfwata mwanaume nyumbani kwake, kwahiyo kama mimi nimemfuata kule, basi mimi nimeolewa kule,” alisema Rama Dee.

Rama Dee akiwa na watoto wake.

 

Katika hatua nyingine Rama Dee amesema hana tofauti yeyote na mbunge wa Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi, alimaarufu kama Mr 2. “Unajua watu wanasema mengi lakini mimi na Sugu tuko poa, hata jana nilikuwa nakunywa soda nay eye sehemu flani hivi”, alisema Rama Dee. Sugu na Rama Dee walidaiwa kutofautiana kutokana na harakati za vinega.

 

Chanzo: Bongo5.com

Leave your comment

Other news