TANZANIA: One More Night ya Jux kufanya vizuri zaidi nje kuliko ndani
23 February 2016

Hapa ndipo usemi usemao ‘Nabii hakubaliki nyumbani kwao unapotimia’, mwanamuziki Juma Jux amedai kuwa video ya wimbo wake wa ‘One More Night’ imekuwa na mafanikio makubwa nje ya nchi kuliko hapa nyumbani.
Msanii huyo amesema amekuwa akipokea comment nyingi nzuri kutoka nje kuhusu video hiyo.
“Video inafanya fresh, inafanya vizuri sana nje kwenye stations kubwa, inapigwa sana. Yaani watu wananiambia kazi ni kubwa na bado naendelea kupata comment nyingi sana kutoka nchi za nje japokuwa wengi hawaelewei lugha”, alisema Jux.
“Pia hata kwa Tanzania kuna baadhi ya mashabiki zangu wanaifurahia sana wanasema nimejaribu kufanya kitu tofauti, sijafanya hivyo before ni kitu kipya, kwahiyo imepokelewa vizuri, video na audio vinafanya poa”, aliongeza Jux.
Video ya One More Night hadi sasa imefikisha views 278,269 kwenye mtandao wa You Tube, tangu ilipotoka mwaka jana mwishoni (Disemba, 2015).
Source: Bongo 5




Leave your comment