TANZANIA: Ni kweli Idriss na Wema Sepetu wameachana? Na kufuta picha za mwenzie kwenye mitandao ya kijamii.

 

 

 

 

Katika wiki chache zilizopita, Idris na Wema Sepetu wameonekana kuwa katika hatua ambayo watu wengi hawakuitegemea kutokea kwa haraka, hatua ya kuuvunja uhusiano wao.

Tetesi za kuvunjika kwa uhusiano wazo zilianza baada ya ujauzito wa Wema kudaiwa kutoka. Haijulikani ni nani amemkosea mwenzie ila wawili hao wamefuta picha na mwenzie katika mitandao ya kijamii (Instagram).

Hapo nyuma Wema aliwahi kueleza jinsi ambavyo alikuwa akimpenda Idris na namna alivyomfanya kuwa mtu mwema.

Hata hivyo inaonekana Idriss bado moyo wake haujakata tamaa kwa mrembo Wema Sepetu, Jumapili alipost picha na kuandika, ‘Only you know how much I love you, the rest doesn’t matter’ #BeingAMan”.

Japo wawili hao walionekana kujibizana katika mtandao wa Snapchat, lakini pia watu wengi walikuwa tayari wameanza kuvutiwa na couple hiyo. Huku wakiwa pia wamepanga kuwa na realityshow yao.

 

Leave your comment