TANZANIA: Q Chief atoa sababu za kutokufanya tena video na director wa ndani!

 

Mwanamuziki Q Chief amesema haoni sababu ya msingi ya kufanya kazi na watayarishaji wa video wa ndani, kwani wanajisifia na kujitapa bila kuwa na lolote.

Msanii huyo ambaye yupo chini ya kampuni ya QSJ Mhonda, amekiambiakipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, kuwa directors wa ndani hawana lolote, hivyo ataenda kufanya kazi nje.

“Kama nina access ya kutoka nje na kufanya mambo yangu ya maendeleo sina haja ya kustick na watu wa bongo, I’ve been here for ten years, kama hukuona kitu nyuma, huwezi kuona kitu sasa”, alisema Q Chief.

“Sio kama nawatukana, lakini naona directors ambao wanajitanua wakati bado, we ukivimba Moe Mussa atafanya nini? Mtoto mdogo wewe hujamfikia hata Tedy Josiah wa Kenya, nyie bado mna changamoto alafu hili mtalielewa, si tunapanda ndege tunaenda kushootia mbali tukirudi tunaachia vyuma, mkijipanga kitabia, mkijipanga kimaisha kimaendeleo production wise, we will come alafu mtataja bei zenu mil 17 tutalipa tutashoot”, aliongeza msanii huyo.

Q Chief amewataka waongoza video wa ndani wajifunze zaidi na kuachana na tamaa ya kutaka malipo makubwa toka kwa wasanii, kwasababu wanaharibu ndoto za wasanii.

Leave your comment