TANZANIA: Ali Kiba na Marijani waangukia mikononi mwa Mapromota matapeli!
23 February 2016

Mapromota feki wanaongezeka kila siku, Jumamosi iliyopita Promota mmoja huko Mombasa, Kenya alitumia jina la Ali Kiba kuwa angetumbuiza siku ya Valentine’s day katika club ya Mnarani ya jijini humo, na wasanii wengine kama Susumila na Tricky B.
Baada ya kugundua hilo, Kiba aliandika kupitia ukurasa wake wa Instagram “Habari Mombasa, Kilifi Malindi. Hii habari sio ya ukweli ni matapeli wanadanganya watu ..na sio kweli, alienunua ticket akadai pesa yake. Sina Show”.
Tukio kama hilo pia lilitokea huko Nairobi, kwake Marijani ambapo JamDown Promoters walipotumia jina lake kutangaza kuhusu show ya kabla ya Valentine day katika ukumbi wa G Club, na kutotokea siku ya show lakini bado waliendelea na show kwa kutumia jina lake.
“Tulikubaliana na mmoja wa promota, Shappa wa JamDown lakini akanitupia mbali katika dakika za mwisho, ingawa nilisafiri kutoka Eldoret kuja kwenye show” alilalamika Marijani.
Kwa mujibu wa Marijani, jithada za kumpata promota huyo hazikuzaa matunda kwasababu hakupokea simu yake (Shappa).Lakini Shappa alivotafutwa na mtandao wa SDE wa Kenya alidai alikuwa amelewa na angemalizana na Marijani muda sio mrefu.




Leave your comment