TANZANIA: Je, kuna uwezekano wa Ali Kiba kufanya kazi na Fergie wa Black Eyed Peas (Marekani)?
23 February 2016

Staa wa muziki Tanzania, Ali Kiba amesema kuna uwezekano wa kufanya kazi na msanii wa Marekani,Fergie anayeunda kundi la Black Eyed Peas.
Akiongea kwenye kipindi cha Chill na Sky, Kiba amesema Novemba mwaka jana kwenye party ya Wild Aid jijini Los Angeles, aliweza kuzungumza na msanii huyo pamoja na mastaa wengine akiwemo Maggie Q.
“Tuliongea na Fergie na akawa yupo interested kufanya nyimbo na mimi baada ya kuona performance yangu”, alisema Ali Kiba.
“Niliperform vizuri pale kwasababu wimbo nilioperform vile vile ilikuwa ni Lupela ambapo kesho yake nikawa nimeshoot video”, aliongeza.
“Anything can happen wewe just hold on”
Ingawa alipata mafanikio na kundi la ‘The Black Eyed Peas’, Fergie ametamba na vibao vyake binafsi kama Glamorous aliomshirikisha Ludacris.
Pia Kiba ameongelea kukutana na Lupita Nyong’o ambaye pia ni balozi wa Wild Aid, amemuelezea kama ni msichana wa pekee.
“She is so lovely” amesema.
“She is so nice yaani, anajielewa sana na she is so proud of Africa, she is very proud nan chi yake ya Kenya, East Africa actually”.




Leave your comment