TANZANIA: Idris Sultan alikuwa akitarajia kupata twins? Soma hapa alichokiandika..

Mshindi wa Big Brother 2014, Idris Sultan ameandika maneno ya uchungu na huzuni kuelezea masikitiko yake chini ya picha inayoonesha watoto mapacha.

Idriss ambaye yupo katika mahusiano na staa wa Bongo movie na aliyekuwa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu. Wiki chache zilizopita walikiri kuwa katika mahusiano na kueleza kuwa wanatarajia kupata mtoto, lakini kwa bahati mbaya mimba hiyo imeharibika.

Soma hapa alichokiandika kupitia ukurasa wake wa Instagram;

Maneno hayo kwa kiswahili;

Kwa mapacha wangu ambao bado walikuwa hawajazaliwa'

“Ni kwa haraka sana mmeingia katika maisha yetu, kwa haraka pia mmetuacha.

Sikuwahi kupata nafasi ya kuonanan na ninyi, kuna ving nataka kusema. Mawazo yote haya yanapita kichwani mwangu,  yanatosha kunifanya kichaa.

Japo mliishi kwa wiki 13 tu, tuliwapenda sana. Natamani ningepata nafasi ya kuwaona na kuwashika. Naimani tutakutana katika maisha mengine.  Mungu ametoa na ametwaa, hatuwezi kulalamika ila kuomba kuwa ilikuwa kwasababu na mipango mizuri kwa ajili yetu hapo baadaye. Kwa uchungu tumejifunza  lakini pia hatutoacha kujaribu tena na tena, naomba kaka na dada zako watakapokuja katika ulimwengu huu tutakuwa zaidi ya tayari kwa ajili yao”

 

 

 

Leave your comment