TANZANIA: Baba wa Diamond asema alitambulishwa Wema Pekee.
12 February 2016

Baba mzazi wa nyota wa muziki Diamond Platnumz, Abdul Juma amedai Wema Sepetu ndiye mwanamke pekee ambaye mwanae Diamond aliweza kumtambulisha kwake kama mpenzi wake.
Akizungumza katika kipindi cha The Weekend Chat Show cha Clouds TV, Mzee Abdul alidai Diamond alimtambulisha Wema kwake pamoja na kumvalisha pete.
“Yaan Diamond toka akiwa na Wema ndio alikuja hapa kumvalisha pete’, alisema Mzee Abdul.
“Unajua toka nizaliwe sijawahi kuona mwanamke mwenye heshima zake kama Wema, nimewahi kuletewa mwanamke mmoja tu toka (Diamond) anakuwa”.
Na pa aliongeza, “Only one hana umalaya huo. Kwasababu mimi Diamond namwamini kitu kimoja, muda wa kutembelea kwenye madisko hana. Yeye ni mtu wa kukaa nyumbani kufikiria anafanya nini kwasababu mwenyewe anajiona yupo kwenye ushindani, bila kujiandaa kwa kazi zijazo ‘atarostika’. Kwahiyo mimi nasema big up akaze buti”.




Leave your comment